Waliosababisha vifo vya askari 70 wasakwa

0
607

Jeshi nchini Niger linawatafuta wapiganaji wenye silaha ambao inasemekana wamefanya mashambulio nchini humo na kusababisha vifo vya askari Sabini wa jeshi la nchi hiyo.

Habari kutoka nchini Niger zinasema kuwa, watu hao wenye silaha walishambulia kambi moja ya kijeshi nchini humo iliyoko huko Tillaberi, eneo ambalo nchi hiyo inapakana na nchi ya Mali na kusababisha vifo vya askari hao huku wengine kadhaa wakijeruhiwa.

Hadi sasa hakuna kikundi chochote kilichodai kuhusika na shambulio hilo, lakini wapiganaji wa kikundi cha IS wenye uhusiano wa karibu na kikundi cha Al Qaeda mara kadhaa wamehusika katika mashambulio ya kigaidi katika eneo hilo la Afrika ya Kaskazini.