Walionacho wakumbushwa kuwajali wasio nacho

0
265

Askofu wa Jimbo Katoliki la Tunduru – Masasi Filbert Mhasi amewakumbusha
Watanzania walionacho kuwa sehemu ya furaha, upendo na amani kwa wengine ambao hawajajaliwa kuwa nacho na wanaoteseka kwa kukosa mahitaji mbalimbali.

Askofu Mhasi ametoa wito huo wakati wa adhimisho la Misa Takatifu ya Jumamosi Kuu iliyofanyika katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Francis Xaveri Tunduru, Ruvuma.

Amesema kuna watu wana mali na wanoishi maisha ya kifahari
na wamesahau Mungu aliwapa mali hizo ill nao wawakumbuke na kuwasasaidia wasio nacho.

“Yesu Kristo Mfufuka hakukata tamaa katika kumkomboa mwanadamu mwenye kila aina ya dhambi, hivyo ufufuko wake ukawe mwanga, furaha na upendo kwa wale wanaotekesa kwa sababu ya kukosa chakula na mahitaji mengine muhimu,”, amesema Askofu Mhasi

Pia amewakumbusha Wazazi na Walezi nchini kutumia Ufufuko wa Yesu Kristo kuwasaidia watoto katika makuzi yao, ili kuwanusuru na changamoto za mmomonyoko wa maadili