Idadi ya watu waliofariki dunia baada ya moto kuzuka katika wodi ya wagonjwa wa corona kwenye hospitali ya A l- Hussein iliyopo katika mji wa Nasiriya nchini Iraq imefikia 92.
Moto huo umezuka baada ya mitungu iliyokuwa imehifadhi hewa ya Oksijeni inayotumiwa na wagonjwa hao wa corona kulipuka.
Waziri Mkuu wa Iraq, Mustafa Al-Kadhimi ameahidi Serikali yake kuchukua hatua za haraka dhidi ya wale wote waliohusika na tukio hilo, kwani hii ni mara ya pili moto kutokea katika wodi za wagonjwa wa corona na kusababisha maafa.
Moto mwingine kama huo ulizuka mwezi Aprili mwaka huu.
Ndugu wa wagonjwa waliolazwa hospitalini hapo wamekwenda katika eneo la tukio kusaidia zoezi la uokoaji, ili hatimaye wajue hatma ya ndugu zao ambao hawajulikani walipo hadi sasa.