Baadhi ya Wakimbizi wa jamii ya Rohingya wanaoishi katika kambi ya Wakimbizi nchini Bangladesh wamesema kuwa, hawaoni matokeo ya Kiongozi wa Myanmar, – Aung San Suu Kyi kwenda kutoa utetezi wake kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu huko The Hague.
Wakimbizi hao waliolazimika kuishi nchini Bangladesh kwa madai kuwa jeshi la Myanmar lilihusika na mauaji ya kimbari nchini mwao dhidi ya watu wa kabila hilo wamesema kuwa, Suu Kyi hata siku moja hawezi kuwatetea.
Wameongeza kuwa, licha ya kuahidi kuwa serikali yake itachukua hatua madhubuti dhidi ya watu waliohusika na mauaji ya watu wa jamii ya Rohingya, lakini kwao hatua hiyo haiwasaidii kwani wanaishi kama Wakimbizi, huku wakiwa hawana matumaini ya mustakabali wa maisha yao.
Wanasema kuwa, Suu Kyi hawezi kwenda kinyume cha jeshi ambalo lilimuweka madarakani.