Wagonjwa wakosa huduma Venezuela

0
335

Baadhi ya Raia wa Venezuela wameanza kwenda kwa waganga wa kienyeji nchini humo, ili kutafuta tiba baada ya Taifa hilo kujikuta kwenye mgogoro mkubwa wa kisiasa, hali iliyosababisha nchi hiyo kukosa huduma muhimu za kijamii.


Baadhi ya wagonjwa wakiwemo wale wanaosumbuliwa na maradhi ya saratani wamesema kuwa, wamelazimika kwenda kwa waganga wa kienyeji kutafuta tiba, ili kupunguza maumivu ya magonjwa yao kwa vile wanashindwa kupata tiba na dawa katika hospitali.


Venezuela imejikuta katika mgogoro wa kisiasa baada ya kiongozi wa upinzani nchini humo Juan Guido kujitangaza kuwa ndiye Rais wa serikali ya mpito ya nchi hiyo na kutambuliwa na nchi za Magharibi ikiwemo Marekani.


Hali hiyo imesababisha mgogoro mkubwa wa kisiasa nchini humo, ambapo Jumuiya ya Kimataifa imekuwa ikimshinikiza Rais Nicolas Maduro wa nchi hiyo kuachia madaraka, huku nchi za China, Russia na Cuba zikimuunga mkono mwanasiasa huyo.