Wafariki kwa kupigwa Risasi

0
393

Watu sita wamekufa na wawili kujeruhiwa vibaya baada ya kupigwa risasi na  mtu mmoja katika hospitali  ya  Ostrava katika Jamhuri ya Czech(chek).

Polisi nchini humo imesema tayari imempata muuwaji huyo ambaye walimkuta ndani ya gari akiwa tayari amekufa baada ya kujipiga risasi huku ulinzi mkali ukiwa umeimarishwa katika hospitali hiyo.

Tukio linaelezwa kutokea katika wodi ya wagonjwa wenye matatizo ya akili  ndipo muuwaji huyo alipoanza kuwapiga risasi watu waliokaribu nae.

Rais Milos Zeman wa nchi hiyo pamoja na Waziri Mkuu Andrej Babis wametoa pole kwa familia za marehemu na majeruhi ambao wapo hospitalini na kusema uchunguzi juu ya tukio hilo unafanyika.