Wafanyakazi wa Twitter wafungiwa nje

0
1131
SAN FRANCISCO, CA - NOVEMBER 04: Twitter headquarters stands on 10th Street on November 4, 2022 in San Francisco, California. Twitter Inc reportedly began laying off employees across its departments on Friday as new owner Elon Musk is reportedly looking to cut around half of the company's workforce. (Photo by David Odisho/Getty Images)

Twitter imewataarifu wafanyakazi wake kuwa wanafunga majengo yake, hivyo hakuna atakayeruhusiwa kuingia humo.

Taarifa hiyo imekuja kipindi ambacho wafanyakazi wengi wamekuwa wakiacha kazi baada ya Elon Musk ambaye ni mmiliki mpya kuwataka wasaini kufanya kazi kwa muda mrefu ama waondoke.

Bila kupewa sababu yoyote, wafanyakazi walipewa taarifa kuwa ofisi hizo zitafunguliwa Jumatatu ya Novemba 21, 2022.

Aidha, wafanyakazi hao wametakwa “kuzingatia sera ya kampuni kwa kuacha kujadili taarifa za siri za kampuni kwenye mitandao ya kijamii, na waandishi wa habari au mahali pengine popote.”

Musk ameonekana akituma jumbe tata kwenye ukurasa wa Twitter lakini pia aliweza kujibu kuhusiana na wafanyakazi kuacha kazi kwa wingi kwa kusema, “Watu bora wanakaa, kwa hivyo sina wasiwasi sana.”

pic.twitter.com/rbwbsLA1ZG— Elon Musk (@elonmusk) November 18, 2022

Musk ambaye ndio tajiri namba moja duniani alinunua Twitter mwezi uliopita kwa mkataba wa dola za Kimarekani bilioni 44, sawa na takribani trilioni 102. 61 za Kitanzania.