Waasi wa kundi la ADF wameshambulia tena mji wa Beni katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, na kuuwa watu 22 katika eneo la Ndombi na Kamango.
Waasi hao wanaelezwa kuwashambulia wakaazi hao kwa risasi na kuwauawa wakiwemo wanawake na watoto huku wengine wakijeruhiwa hata hivyo jeshi la nchi hiyo liliingilia kati na kupambana na waasi hao.
Mwenyekiti wa mashirika ya kutetea haki za binaadamu Cepadho Omar Kavota amelalamikia jesh la nchi hiyo kwa kushindwa kuwatokgomeza waasi wa ADF.
Zaidi ya watu 100 wameuwawa katika mashambulizi yanayodaiwa kufanywa na kundi hilo tangu Novemba 5 mwaka huu wakati huohuo viongozi wakuu wa nchi za Sahel wanakutana nchini Niger kujadili na kupatia ufumbuzi mashambulizi yanayoendelea katika maeneo ya ukanda huo ambayo yamekuwa yakijitokeza mra kwa mara.