Waandamanaji wafunga barabara kutoka Hispania kwenda Ufaransa

0
778

Waandamanaji katika jimbo la Catalonia nchini Hispania wanaopigania jimbo lao kujitenga, kwa siku ya Pili hii leo wamefunga tena barabara kuu kutoka nchini humo inayoelekea katika nchi jirani ya Ufaransa.

Waandamanaji hao wanasema kuwa, wamekasirishwa na hatua ya Serikali ya Hispania kuwatia mbaroni na kuwafunga Viongozi wa jimbo hilo wanaotetea jimbo la Catalonia kujitenga kutoka katika Serikali Kuu ya Hispania.

Watu hao wameweka vizuizi vya barabarani pamoja na kuegesha vibaya magari katika barabara hiyo ili kuzuia shughuli za usafiri katika eneo hilo.