Viongozi wa maandamano katika jimbo la Hong Kong nchini China hivi sasa wameelekeza maandamano yao ya kupinga serikali dhidi ya vyombo vya usalama nchini humo, hasa askari wa kulinda usalama.
Waandamanaji hao wamekwenda hadi katika makao makuu wa wizara ya sheria na polisi wamelazimika kwenda katika eneo hilo kuzuia maandamano yao, kwani haifahamiki waandamanaji wanataka kufanya nini katika eneo hilo.
Waandamanaji wamekasirishwa na mpango wa serikali ya nchi yao wa kupitisha muswada wa kuwapeleka watuhumiwa kutoka katika kisiwa cha Hong Kong kwenda kushitakiwa, bara ya China.
Licha ya serikali ya China kutangaza kuahirisha kupitisha muswada huo, waandamanaji wanasisitiza kuwa hatua hiyo haitoshi wanachotaka ni muswada huo kutupiliwa mbali na serikali.