Visa vya Corona vyaongezeka Afrika Kusini

0
411

Waziri wa Afya wa Afrika Kusini, ametangaza visa vya COVID-19 kuongezeka nchini humo, huku vifo navyo vikiongezeka hadi 194 ikiwa imeongezeka kwa 8 tangu mara ya mwisho kutangaza.

Barani Afrika, Afrika Kusini ndio nchi iliyoathirika zaidi na homa hii ya Corona.

Waziri Zwelini Mkhize amesema vifo nchini humo vimefikia 10, 015.

Kwa upande mwingine nchi hiyo imeanza kulegeza kamba taratibu katika sheria zilizowekwa za kufunga nchi mwezi Machi.