Virusi vya Corona vyaingia Algeria

0
434

Waziri wa Afya wa Algeria amethibitisha kuwepo kwa mtu mmoja aliyebainika kuwa na virusi vya Corona nchini humo, na kwamba tayari hatua za makusudi zimeshachukuliwa.

Katika taarifa aliyoitoa Februari 25, 2020, Waziri Abdel Rahman Ben Bouzid ameeleza kuwa muathirika huyo ni raia wa Italia ambaye aliwasili nchini humo Februari 17, na tayari amewekwa kwenye eneo maalumu kwa matibabu.

Algeria inakuwa nchi ya pili barani Afrika kuthibitisha kuwa na mtu aliyeathiriwa na virusi hivyo, baada ya Misri kutangaza kuwepo kwa mgonjwa, na baadae walitangaza kuwa amepona.

Hadi sasa nchini Italia kumeripotiwa kuwepo kwa visa 325, vifo 11, na watu wawili waliopona.