Viongozi mbalimbali walia na vikwazo nchini Zimbabwe

0
841

Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) zimetakiwa kushirikiana ili kukabiliana na vikwazo vya kiuchumi ilivyowekewa Zimbabwe na nchi za Magharibi.

Kauli hiyo imetolewa jijini Dar es salaam na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto mwenye dhamana ya Maendeleo ya Jamii Dkt John Jingu, wakati wa kongamano maalum lililokua na lengo la kujadili vikwazo vya kiuchumi na hatma ya maendeleo ya Afrika, mikakati ya kuikwamua Afrika katika ukoloni mamboleo na nafasi ya SADC katika mapambano dhidi ya vikwazo vya kiuchumi nchini Zimbabwe.

Dkt Jingu amesisitiza kuwa, aina zote za Ubeberu Barani Afrika ni lazima zipingwe kwa nguvu zote.

Kwa upande wake Waziri Mkuu Mstaafu Joseph Warioba amesema kuwa, Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alikuwa miongoni mwa viongozi wa Afrika waliofanya jitihada kubwa katika kupinga Ubeberu, hivyo ni muhimu jitihada zake zikaenziwa.