Viongozi EAC kuijadili DRC

0
131

Viongozi wa mataifa saba yanayounda Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) wanatarajiwa kukutana hii leo jijini Nairobi, Kenya, kujadili hali ya usalama katika eneo la mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.

Mkutano huu unafanyika kufuatia kuzuka kwa mapigano baina ya DRC na Rwanda, huku DRC ikiilaumu Rwanda kutokana na kuibuka upya hivi karibuni kwa kundi la waasi la M23.

Rwanda imekanusha kuwaunga mkono waasi hao , huku nchi zote mbili zikilaumiana kwa kufanya mashambulizi ya kuvuka mpaka.