Vikosi vya Serikali ya Russia vinashutumiwa kufanya mashambulio ya anga katika mji wa Idlib nchini Syria, mashambulio yaliyolenga hospitali moja katika mji huo.
Habari zinasema watu kadhaa wameuawa katika shambulio hilo, wengi wakiwa ni Wanawake na Watoto.
Majeshi ya Russia yako nchini Syria kuisaidia Serikali ya Rais Bashar Al Assad wa nchi hiyo, anayepambana na vikundi mbalimbali vya Wanamgambo wakiwemo wale wa IS waliodhamiria kumuondoa madarakani.