Vikosi vya kulinda amani vyamaliza jukumu lake Darfur

0
164

Vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika katika jimbo la Darfur nchini Sudan, vimekamilisha rasmi jukumu hilo, baada ya kulinda amani kwa takribani miaka 13.

Vikosi hivyo vilipelekwa katika jimbo la Darfur kwa ajili ya kuwalinda raia wa jimbo hilo pamoja na kusaidia kutoa misaada mbalimbali baada ya kuwepo kwa mapigano ya muda mrefu.

Mapigano hayo yalikuwa baina ya vikosi vya Serikali na Wanamgambo wa Janjaweed, ambao wanashutumiwa kwa kufanya mauaji ya kikatili kwa raia wasio na hatia, shutuma ambazo wamekuwa wakizikanusha.