Uuzaji wa silaha

0
423

Wizara ya mambo ya nje nchini Marekani imeidhinisha uuzaji wa silaha kwa Taiwan, utakaogharimu $2.2bn .


Mpango huo ni wa vifaru 108 , makombora 250 na vifaa vyengine vya kijeshi.


Mwezi uliopita wizara ya maswala ya mambo ya nje ya China iliitaka Marekani kusitisha uuzaji huo , ukiutaja kuwa ni uamuzi mbaya.


China inalichukulia eneo la Taiwan kuwa miongoni mwa himaya yake ambapo msemaji wake wa wizara ya mambo ya nje Geng Shang ameitaka Marekani kuheshimu sera ya China ya taifa moja na kusisitiza kuwa Uuzaji wa silaha hizo hautaathiri uwezo wowote wa kijeshi katika eneo hilo.


Oparesheni hiyo inakuja siku chache baada ya wizara ya mambo ya nje ya China kuionya Marekani kupinga uhuru wa China katika eneo hilo.