Uturuki kuendeleza mashambulio dhidi ya Syria

0
255

Rais Recep Tayyip Erdoğan wa Uturuki amesema kuwa majeshi ya nchi hiyo yataendeleza mashambulio dhidi ya majeshi ya Syria katika Jimbo la Idlib, licha ya nchi hiyo awali kuahidi kurejesha nyuma majeshi hayo.

Uturuki imesema kuwa itafanya mashambulio ya mara moja endapo majeshi yake yatakuwa hatarini huko Idlib kwa ajili ya usalama wa askari wake na Taifa hilo kwa ujumla.

Erdoğan amesema kuwa, matakwa ya nchi yake hayajatekelezwa na serikali ya Russia kama nchi hizo zilivyokuwa zimekubaliana awali katika mazungumzo.

Majeshi ya Russia yako nchini Syria kuyasaidia majeshi ya nchi hiyo yanayopigana dhidi ya waasi waliodhamiria kumuondoa madarakani Rais Bashar Al Assad kwa miaka kadhaa sasa.

Majeshi ya Uturuki yalitangaza kuingia nchini Syria kuwasaka waasi wanaopigana dhidi ya serikali ya nchi hiyo baada ya majeshi ya Marekani yaliyokuwa yakilinda amani nchini Syria kutangaza kuondoka.