Upinzani Msumbiji walalamikia matokeo ya awali ya uchaguzi

0
800

Upande wa upinzani nchini Msumbiji, umeanza maandamano ya kupinga matokeo ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika hivi karibuni, baada ya matokeo ya awali kuonyesha kuwa chama tawala nchini humo cha FRERIMO kinaongoza.

Kwa mujibu wa matokeo hayo, Rais Filipe Nyusi wa Msumbiji huenda akapata ridhaa ya kuliongoza Taifa hilo kwa muhula mwingine.

Wapinzani wanadai kuwa kumekuwa na ukiukwaji wa taratibu za uchaguzi na kura za upinzani kuibwa.

Habari kutoka nchini Msumbiji zinasema kuwa, tangu nchi hiyo ipate uhuru, hakuna matokeo ya uchaguzi yaliyowahi kukubaliwa mara moja na upande wa upinzani, na mara kadhaa upande huo umepinga matokeo na kuandamana baada ya chama tawala kushinda.