UN yaomba msaada kwa ajili ya Yemen

0
554

Umoja wa Mataifa umewaomba Wafadhili kuchangia Dola Bilioni 4.2 za Kimarekani  kwa ajili ya msaada kwa Yemen, ambako watu Milioni 20 wanakabiliwa na uhaba wa chakula.

Ombi hili limetolewa Geneva, -Uswisi na wawakilishi wa Umoja wa Mataifa wakati wa mkutano unaowashirikisha Wafadhili wa Kimataifa kwa lengo la kuchangisha fedha kwa ajili ya kuisaidia Yemen.

Umoja wa Mataifa umepanga kukusanya kiasi hicho cha fedha kwa ajili kununua chakula cha raia Milioni 12 wa Yemen katika kipindi cha mwaka huu, kununua maji ya kunywa pamoja na dawa.

Mwaka 2018  Umoja wa Mataifa uliowaomba Wafadhili wa Kimataifa kuupatia Dola Bilioni Tatu za Kimarekani na ulipokea asilimia 83 ya fedha hizo kwa ajili ya kuisaidia Yemen.