Umoja wa mataifa umelaani matumizi ya watoto wadogo katika mashambulio ya mabomu ya kujitoa muhanga kama mchango
Hatua hiyo ya Umoja wa mataifa inafuatia matukio ya milipiko ya kujitoa muhanga iliyotokea katika kijiji cha Konduga kaskazini mwa Nigeria na kusabasisha vifo vya watu takribani thelathini.
Tayari jeshi la polisi nchini humo linamshikilia mtu mmoja anayedaiwa kuhusika na milipuko hiyo huku kundi la Boko haram likidaiwa kuhusika kupanga mashambulio hayo.