Uingereza yatangaza kuwaweka karantini wasafiri

0
479

Uingereza imetangaza kuwaweka karantini kwa siku 14 wasafiri wanaoingia nchini humo kutoka nchi kadhaa ikiwemo Ufaransa,Uholanzi, Monaco, Malta, Aruba kuanzia hapo kesho siku ya Jumamosi.

Uamuzi huo umefikiwa baada ya kuripotiwa kwa maambukizi mapya ya Covid 19.

Habari zinasema kuna raia wengi wa Uingereza waliokuwa wamekwenda nchini Ufaransa kwa mapumziko huku, baadhi ya kampuni za usafiri zikisema hazitamudu kusafirisha abiria wote watakaotaka kwenda nchini Uingereza kabla ya kuanza utekelezaji wa karantini hiyo.