Uingereza waanza kupiga kura

0
489

Wananchi wa Uingereza wameanza kupiga kura katika uchaguzi mkuu wa nchi hiyo ili kuamua ni nani atakayeliongoza Taifa hilo katika muhula mwingine.

Huo ni uchaguzi wa Tatu kufanyika nchini Uingereza katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, changamoto kubwa ikiwa ni hatua ya nchi hiyo kutaka kujitoa rasmi kwenye Umoja wa nchi za Ulaya.

Hatua hiyo tayari imesababisha Mawaziri Wakuu Watatu kuachia madaraka akiwemo Waziri Mkuu wa sasa Borris Johnson, ambaye moja kwa moja ameingia katika kinyang’anyiro cha kutetea nafasi yake.

Huo ni uchaguzi wa kwanza pia kufanyika nchini Uingereza mwezi Disemba, kwani mwezi huu mara nyingi huwa ni muda wa sherehe na mapumziko ya Krismasi na mwaka mpya.