Uganda yatangaza kuwarejesha raia 22 kwenye nchi zao

0
645

Serikali ya Uganda imeamuru raia 22 wa kigeni kurejea katika nchi zao, baada ya kukataa kuwekwa katika karantini ili kubaini kama wameambukizwa virusi vya corona ama la.

Waziri wa Afya wa Uganda, – Jane Ruth Aceng amesema kuwa serikali ya nchi hiyo haitaruhusu raia hao kuendelea kuwepo nchini humo kama hawatakubali kukaa katika karantini,  kwa kuwa baadhi yao wametoka kwenye nchi ambazo tayari zina mlipuko wa virusi vya corona.

Raia hao wanatoka katika nchi za Italia,  Iran, Korea Kusini, Ufaransa, China, Ujerumani na Hispania,  na waliwasili nchini Uganda kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa kimataifa wa  biashara.

Serikali ya Uganda imeagiza wageni wote wanaoingia nchini humo kuwekwa katika karantini kwa muda wa siku kumi na nne ili kubaini kama wameambukizwa virusi vya corona ama la.