Serikali ya Uganda imeridhia kuundwa kwa Baraza la Kiswahili la Taifa, litakalosimamia kurasimishwa kwa Kiswahili kuwa lugha ya pili ya Taifa hilo.
Msemaji wa Serikali ya Uganda, -Ofwono Opondo amesema kuwa, uamuzi wa kuundwa kwa Baraza hilo la Kiswahili la Taifa umeridhiwa katika kikao cha Baraza la Mawaziri la nchi hiyo.
Amesema kuwa, kazi kubwa ya Baraza hilo itakua ni kuhakikisha lugha ya Kiswahili inakuwa lugha rasmi ya Pili nchini Uganda baada ya lugha ya Kiingereza.
Baraza hilo la Kiswahili la Taifa la Uganda pia litasimamia kubuniwa kwa Sera, Mwongozo na kuweka mikakati ya kuhakikisha kuwa lugha ya Kiswahili inafundishwa katika maeneo mbalimbali nchini humo.