Uganda waendelea kupiga kura

0
165

Wananchi wa Uganda wanaendelea kupiga kura kumchagua Rais pamoja na Wabunge.

Habari kutoka nchini Uganda zinaeleza kuwa, kumekuwa na misururu mirefu ya wapiga kura hasa katika mji mkuu wa Uganda, – Kampala, hali inayoashiria watu wengi wamejitokeza kupiga kura hata katika maeneo mengine.

Vituo vya kupigia kura vilivyofunguliwa saa moja asubuhi, vinatarajiwa kufungwa saa kumi kamili jioni.

Rais Yoweri Museveni anayewania kiti cha Urais kwa mara nyingine tena, alitarajiwa kupiga kura nyumbani kwake huko Magharibi mwa Uganda.

Mgombea Urais wa upande wa upinzani Bobi Wine, yeye alitarajiwa kupiga kura katika moja ya vituo vilivyopo mjini Kampala.

Rais Museveni anayewania kiti cha Urais kwa kipindi cha sita, tayari amekaa madarakani kwa takribani miaka 35.