Polisi nchini Lesotho wamesema wana ushaidi wa kutosha kwamba aliyekuwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo Thomas Thabane kwa kushirikiana na mke wake wa sasa Maesaiah Thabane waliwalipa watu ili wamuue mke wa zamani wa Thabane, – Lipolelo Thabane.
Mwaka 2017 Lipolelo alipigwa risasi na kufariki dunia usiku wa kuamkia siku ya kuapishwa kwa Thabane kuwa Waziri Mkuu.
Taarifa ya polisi nchini Lesotho imepinga ombi la Maesaiah la kutaka aachiwe kwa dhamana baada ya kuzuiliwa tangu wiki iliyopita.
Mawakili wa Maesaiah wanataka mteja wao aachiwe kwa dhamana ili akamhudumie mume wake Thabane ambaye kwa sasa ni mgonjwa