Trump atoa tahadhari

0
782

Rais wa Marekani Donald Trump ametahadharisha wananchi wake kuwa nchi yake imeingia katika wiki ngumu zaidi kufuatia kuongezeka kwa kasi ya maambukizi ya virusi vya Corona kwa wananchi nchini humo.

Watu zaidi ya Laki Tatu wameathirika kutokana na maambukizi ya Virusi vya Corona
nchini Marekani huku Rais Trump akisema huenda hali ikawa mbaya zaidi kati ya wiki hii na wiki ijayo.

Zaidi ya watu Elfu nane wamekufa kutokana na Maradhi ya Corona huku Jumamosi
ikiripotiwa vifo 630 na kuendelea kutishia maisha ya wananchi nchini humo na duniani kwa ujumla.

Jimbo la New York pekee limeandikisha vifo zaidi ya 3500 kati ya Elfu nane wakati huko
nchini Italia, idadi ya vifo imeongezeka na kufikia 15,362 wakati Hispania ikiripoti jumla ya vifo 11,744.

Takwimu zilizokusanywa na Chuo Kikuu cha John Hopkins zinadokeza kuripotiwa vifo
Elfu sitini ulimwenguni kote huku maambukizi yakifikia zaidi ya watu Milioni moja