Trump aondolewa mashtaka

0
377

Baraza la Seneti nchini Marekani limemuondolea Rais Donald Trump wa nchi hiyo mashtaka yaliyokua yakimkabili, na hivyo kumaliza mchakato wa kumuondoa madarakani.

Baraza hilo linaloongozwa na Chama Cha Republican cha Rais Trump, lilipiga kura 52 dhidi ya 48 kuhusu mashtaka ya matumizi mabaya ya madaraka na kura 53 dhidi ya 47 kuhusu mashtaka ya kuzuia bunge kufanya kazi yake.

Rais Trump alikua akikabiliwa na tuhuma za kuishinikiza Ukraine kumchunguza kwa siri mpinzani wake wa kisiasa Joe Biden.

Endapo angekutwa na hatia kwa kosa lolote kati ya hayo, Trump angelazimika kukabidhi madaraka yake kwa Makamu wa Rais  wa nchi hiyo Mike Pence.