Trump afuta mazungumzo yake na Wanamgambo wa Taliban

0
461

Rais Donald Trump wa Marekani, amefuta mazungumzo yaliyokua yafanyike kati yake na Wanamgambo wa Taliban wa nchini Afghanistan, kwa lengo la kumaliza vita vilivyodumu kwa muda wa miaka 18 nchini humo.

Katika mtandao wake wa kijamii wa twitter Trump ameandika kuwa, alipanga kukutana na Rais   Ashraf Ghani wa Afghanistan pamoja na viongozi wa ngazi ya juu wa Wanamgambo hao nchini Marekani hii leo, lakini hatafanya hivyo.

Habari zaidi zinaeleza kuwa Trump amefuta mazungumzo hayo ambayo yangekua ya siri, baada ya Wanamgambo hao wa Taliban kudai kuhusika na shambulio la hivi karibuni mjini Kabul, shambulio lililosababisha vifo vya watu 12 akiwemo askari mmoja wa Marekani.