Trudeau ashinda Canada

0
741

Chama cha Liberal nchini Canada kimefanikiwa kuendelea kubaki
madarakani kwa ushindi mdogo katika uchaguzi uliofanyika nchini humo.

Kufuatia ushindi huo Justin Trudeau atakuwa Waziri Mkuu wa  serikali
yenye wawakilishi wachache bungeni.

Chama cha Liberal kinakadiriwa kupata viti 157 ikiwa ni viti 13
pungufu ya idadi ya wabunge wengi wanaotakiwa.Hatua hiyo itasababisha
chama hicho kukabiliwa na ugumu katika upitishaji wa miswada ya sheria
katika muhula wa pili wa uongozi wa Trudeau.

Chama cha upinzani cha Conservative kinatarajiwa kupata viti 121 idadi
hiyo ikiwa imeongezeka kutoka viti 95 ilivyokuwa ikishikilia awali.