Touadéra kuiongoza tena CAR

0
130

Rais Faustin-Archange Touadéra wa Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR), ametangazwa mshindi wa kiti cha Urais kufuatia uchaguzi iliofanyika Desemba 27 mwaka 2020.

Tume ya Uchaguzi katika Jamhuri hiyo imemtangaza Faustin-Archange Touadéra kuwa mshindi baada ya kupata karibu asilimia 54 ya kura zote zilizopigwa, na hivyo kuliepusha Taifa hilo kuingia katika duru ya pili ya uchaguzi.

Kwa mujibu wa matokeo hayo yaliyotangazwa na Tume ya Uchaguzi ya CAR, Waziri Mkuu wa zamani wa Jamhuri hiyo Anicet George Pologuele ameshika nafasi ya pili kwa kupata asilimia 21 na Martin Ziguele amepata asilimia 7 ya kura zote zilizopigwa.

Wagombea 16 walichuana katika kinyang’anyiro cha Urais, huku Wanawake wakiwa watatu.