Zaidi ya watu elfu mbili wamefariki dunia na wengine wengi wanaendelea na matibabu baada ya tetemeko la ardhi kuikumba Afghanistan.
Timu ya waokoaji inaendelea kuwatafuka watu walionaswa katika vifusi vya majengo pamoja na kuwasaidia watu walioathirika ambao wamepoteza makazi yao.
Habari zaidi kutoka nchini Afghanistan zinaeleza kuwa, miundombinu mbalimbali ikiwa ni pamoja na barabara na madaraja imeharibiwa.
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Afghanistan imetoa wito kwa Jumuiya ya Kimataifa kuwasaidia watu walioathirika na tetemeko hilo la ardhi.