Tetemeko la ardhi laitikisha Philippines

0
833

Watu kumi na mmoja wamekufa na wengine kadhaa kujeruhiwa, baada ya tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa vipimo vya matetemeko vya Ritcher Sita Nukta Tano kulitikisa eneo la Miandanao nchini Philippines.

Tetemeko hilo limezusha hali ya hofu katika eneo hilo na kusababisha watu kukimbia hovyo, wakitafuta mahali salama.

Majengo kadhaa yameporomoka baada ya tetemeko hilo, yakiwemo yale ya hospitali, shule na Ofisi.

Hilo ni tetemeko la ardhi la Tatu kutokea nchini Philippines, ndani ya kipindi cha wiki Mbili.