Tanzania yatoa matamko 15 UN

0
166

Matamko15 yametolewa katika mkutano wa 51 wa Baraza la Haki za Binadamu unaoendelea Geneva, Nchi Uswisi.

Tanzania imetoa matamko hayo katika masuala ya Afya, Elimu, Haki, Ardhi, Vijana, Wanawake, Uhuru wa Vyombo vya Habari, Kujenga uwezo kwa wananchi, Maliasili ya Taifa, Uhifadhi, Haki za Wazee, Watoto na Wanawake na Ufanyaji kazi wa Taasisi zisizo za Kiserikali.

Ujumbe wa Tanzania umeongozwa na Katibu Mkuu Maliasili na Utalii Profesa Eliamani Sedoyeka, Mwakilishi wa kudumu wa Tanzania katika Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Geneva Balozi Maimuna Tarishi na Naibu Mwakilishi wa Kudumu UN Geneva balozi Hoyce Temu.