Rais Samia Suluhu Hassan ametaka kuwepo kwa jitihada za pamoja miongoni mwa mataifa mbalimbali duniani, katika kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi.
Rais Samia Suluhu Hassan ametoa wito huo wakati akihutubia mkutano wa wakuu wa nchi wanaoshiriki katika mkutano wa 26 wa Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya Tabianchi (COP26) unaoendelea huko Glasgow, Scotland.
Amesema mabadiliko ya Tabianchi hayachagui nchi tajiri ama maskini, hivyo jitihada za pamoja zinahitajika katika kukabiliana nayo.
Amewaambia washiriki wa mkutano huo kuwa Tanzania kama yalivyo mataifa mengine duniani inafanya jitihada kubwa katika kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi.
Kwa mujibu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Tanzania inafanya hivyo kwa kutambua kuwa nayo imeathirika na mabadiliko hayo ya Tabianchi kama zilivyo nchi nyingine duniani.
Sign in
Welcome! Log into your account
Forgot your password? Get help
Password recovery
Recover your password
A password will be e-mailed to you.