Tanzania kuongeza uwekezaji Kenya

0
233

Tanzania na Kenya zimekubaliana kukuza biashara na uwekezaji baina ya nchi hizo kutokana na nchi hizo kuwa na fursa nyinyi.

Hayo yamesemwa na Rais Samia Suluhu Hassan katika Ikulu ya Kenya jijini Nairobi wakati wa mkutano na Waandishi wa habari,  mara baada ya mazungumzo yake ya faragha na Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya.

Amesema Tanzania na Kenya zitatumia fursa nyingi zilizopo za biashara na uwekezaji katika nchi hizo,  ili kukuza biashara na uwekezaji kwenye nchi hizo na nje ya nchi hizo.

Rais Samia Suluhu Hassan ameongeza kuwa Tanzania itaongeza uwekezaji nchini Kenya, nchi ambayo inashika nafasi ya tano kwa uwekezaji Tanzania miongoni mwa nchi mbalimbali duniani na inashika nafasi ya kwanza kwa nchi za Afrika Mashariki.

Amesema kuwa ni muhimu kwa Tanzania kuendeleza uhusiano wa kibiashara na uwekezaji na Kenya kwa kuwa tayari nchi hiyo imewekeza miradi 513  yenye thamani ya  bola bilioni   1.7  za kimarekani na kutoa ajira zaidi ya elfu 50 kwa Watanzania,

Ameongeza kuwa kampuni 30 za Tanzania zimewekeza Kenya mtaji wenye thamani ya shilingi bilioni 19 za Kenya na kutoa ajira 2, 640.