Tani 3.2 za pembe za ndovu zakamatwa Cambodia

0
1293

Cambodia imekamata tani 3.2 za pembe za ndovu ambazo zimeingizwa kimagendo nchini humo kutoka nchini  Msumbiji.

Habari kutoka nchini Cambodia zimesema kuwa pembe hizo za ndovu 1,206 zimepatikana katika kontena lililokua ndani ya meli moja nchini humo.

Maafisa usalama wa Cambodia wamesema kuwa pembe hizo za ndovu ziliingizwa nchini humo mwaka 2017, lakini mmiliki wake hajajitokeza mpaka sasa kuchukua mzigo wake.

Kwa mujibu wa maafisa hao, waligundua mzigo huo wa pembe za ndovu baada ya kupewa taarifa na ubalozi wa Marekani uliopo katika mji wa  Phnom Penh nchini Cambodia.

Biashara ya kimataifa ya pembe za ndovu ilipigwa marufuku tangu mwaka 1989 baada ya idadi ya tembo kupungua kwa kiasi kikubwa Barani Afrika.