Taliban na Panjshid wazidi kupigana

0
239

Hali ya wasiwasi imezidi kuongezeka katika bonde la Panjshir nchini Afghanstan, baada ya mapigano kuendelea kati ya wakazi wa bonde hilo na askari wa jeshi la Taliban.

Watu walioshuhudia tukio hilo wamesema pande hizo zimeshambuliana kwa bunduki usiku kucha, licha ya asubuhi ya leo, hali kuonekana kama vile ni ya utulivu, baada ya milio ya bunduki kupungua.

Shirila moja la misaada ya kitabibu kutoka nchini Italia limesema limekuwa likihudumia mamia ya majeruhi wa mapigano kutoka katika bonde hilo, wengi wao wakiwa na majeraha ya risasi.

Mapigano kati ya pande hizo mbili yalizuka baada ya mazungumzo kuvunjika kati wa serikali ya Taliban na wakazi wa Panjshir.