T.B. Joshua kuzikwa Julai 11

0
212

Kanisa la aliyekuwa Mhubiri maarufu wa nchini Nigeria, Marehemu Temitope Balogun Joshua, maarufu T.B. Joshua limetangaza kuwa mazishi ya Mhubiri huyo yatafanyika Julai 11 mwaka huu.

Taarifa iliyotolewa na kanisa la Sinagogi la mataifa yote SCOAN, imeeleza kuwa TB Joshua atazikwa karibu na makao makuu ya kanisa hilo mjini Lagos.

Mhubiri TB Joshua alifariki dunia tarehe 5 mwezi huu nchini Nigeria, akiwa na umri wa miaka 57.