Shirika la Afya Dunia (WHO) limetangaza mlipuko wa ugonjwa wa Homa ya Manjano Kusini mwa Sudan Kusini, katika eneo la Kajo-keji, mkoa unaopakana na Uganda.
WHO imetahadharisha kuwa uwezekano wa ugonjwa huo kusambaa kwa watu wengi ni mkubwa kutokana na kurejeshwa nchini humo kutoka Uganda watu walioyakimbia makazi yao.
Aidha, udhaifu wa sekta ya afya nchini humo, marufuku ya kusafiri uliyowekwa kutokana na mlipuko wa virusi vya corona, na mvua zinazoendelea kunyesha ambazo zinatoa mazingira rafiki kwa mbu wanaosambaza ugonjwa huo kuzaliana, zimetajwa kuwa ni sababu zinazoweza kuchangia kusambaa kwa Homa ya Manjano.
Wizara ya afya nchini humo kwa kushirikiana na WHO imetangaza kuzindua kampeni ya kutoa chanjo kwa wananchi katika maeneo yaliyoathirika, na kuanzisha mpango mkakati wa kuhakikisha kuwa wananchi wote wanapatiwa chanjo ifikapo 2022.
Mei 2003 Sudan Kusini ilikumbwa na mlipuko mkubwa wa ugonjwa huo, ambapo visa 178 viliripotiwa na kupelea vifo 27 katika Mkoa wa Imatong.