Sudan kuchunguza mapigano mapya Darfur

0
171

Takribani watu 50 wameuawa na wengine wengi kujeruhiwa, baada ya kuzuka kwa mapigano mapya baina ya vikundi vya kikabila katika jimbo la Darfur nchini Sudan.

Mapigano hayo yametokea katika mji wa El Geneina.

Kufuatia mapigano hayo, Waziri Mkuu wa Sudan, – Abdalla Hamdok ametangaza amri ya kuzuia watu kutembea hovyo katika jimbo hilo la Darfur.

Pia ameunda tume kwenda katika jimbo hilo kuchunguza mapigano hayo.

Mapigano ya wenyewè kwa wenyewe katika jimbo hilo la Darfur yalianza tangu mwaka 2003 na kusababisha vifo maelfu ya watu, huku wengine wengi wakiyakimbia makazi yao.

Mapigano ya hivi karibuni yametokea zikiwa zimepita takribani wiki tatu, baada ya askari wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika waliokuwa wakilinda amani katika jimbo la Darfur kwa muda wa miaka 13, kukabidhi jukumu hilo kwa vikosi vya Sudan.