Sierra Leone yalia na vitendo vya udhalilishaji

0
1070

Rais  Julius Maada Bio wa Sierra Leone ametangaza hali ya hatari  nchini humo kufuatia kukithiri kwa vitendo vya udhalilishaji.

Bio ametangaza hali hiyo baada ya kusomewa takwimu zinazoonesha kuongezeka kwa vitendo hivyo vya udhalilishaji, ambapo viliongezeka mara mbili zaidi mwaka 2018 na kufikia 8,505 katika nchi hiyo yenye watu milioni Saba nukta Tano.

Kabla ya kutangaza hali hiyo ya hatari, Rais Bio alisikiliza shuhuda kutoka kwa watu mbalimbali waliofanyiwa vitendo hivyo vya udhalilisha, ambao pia wamelalamikia adhabu ndogo inayotolewa kwa watuhumiwa wa vitendo hivyo.

Kwa mujibu wa Rais huyo wa Sierra Leone, baadhi ya familia nchini humo zinaendeleza utamaduni wa kukaa kimya na kutozungumza kuhusu vitendo hivyo, hali inayowaacha walengwa wakiwa wameathirika zaidi.

Takwimu zilizotolewa na Jeshi la Polisi nchini Sierra Leone  zinaonesha kuwa Theluthi Moja ya vitendo vya udhalilishaji  nchini humo vilivyoripotiwa vinawahusisha watoto wadogo.