Shule yafungwa baada ya Wanafunzi kukanyagana

0
465

Wizara ya Elimu ya Kenya imeifunga kwa muda wa wiki Moja Shule ya Msingi ya Kakamega, baada ya kutokea  vifo vya Wanafunzi 14 kutokana na kukanyagana.

Waziri wa Elimu wa Kenya, George Magoha amesema kuwa mpaka sasa chanzo cha tukio hilo bado hakijafahamika na uchunguzi unaendelea.

Tukio hilo la Wanafunzi kukanyagana katika shule ya msingi ya Kakamega, limetokea majira ya jioni hapo jana wakati Wanafunzi hao walipokua wakitoka darasani kwenda nyumbani.