Waziri mkuu wa India Narendra Modi amewasihi waandamanaji nchini humo kuwa watulivu na kwamba sheria hiyo mpya ilyopitishwa haijalenga kuwabagua waumini wa dini yeyote.
Modi amezungumza hayo hii leo kufuatia maandamano yanayoendelea nchini humo kwa siku ya tano sasa ambapo waandamanaji wanapinga muswada wenye utata wa uraia.
Muswada huo unaelezwa kutoa msamaha kwa wahamiaji haramu kutoka nchi tatu ambazo ni jirani na India ikiwemo Pakistan, Bangladesh na Afghanistan ila wasiwe Waislamu maelfu.
Wakati huo huo polisi nchini humo wanatuhumiwa kutumia nguvu kuzuia maandamano hayo pamoja na kuingia ndani ya vyuo vikuu na kupiga wanafunzi na kutupa mabomu ya machozi ndani ya madarasa na maktaba za vyuo hivyo.
Watu wanne wameripotiwa kufa na zaidi ya watu mia moja kuumia katika maandamano hayo tangu yameanza.