Sheria Mpya Togo yazuia maandamano

0
385

Wabunge wa Bunge la Togo wamepitisha sheria mpya  inayozuia maandamano ya kisiasa nchini humo, katika kipindi hiki ambapo kumekua na maandamano yanayofanywa mara kwa mara na wafuasi wa upande wa upinzani.

Chini ya sheria hiyo mpya, raia yeyote wa nchi hiyo hatoruhusiwa kuandamana katika barabara kuu , katika  miji mikubwa na nje ya majengo ya serikali.

Pia maandamano hayataruhusiwa kufanyika kabla ya saa tano asubuhi na baada ya saa 12 jioni.

Taarifa iliyotolewa na Serikali ya Togo imesema kuwa, sheria hiyo ina lengo la kudumisha hali ya amani ya nchi hiyo, na kuiepusha nchi hiyo na tishio la vitendo vya kigadi.

Hata hivyo upande wa upinzani nchini Togo umesema kuwa, hatua hiyo inakusudia kutotoa nafasi kwa mtu yeyote kugombea kiti cha urais na kuendeleza utawala wa kifamilia.

Katiba ya sasa ya Togo inamruhusu Rais Faure Gnassingbé wa nchi hiyo kushika wadhifa huo hadi mwaka 2030, ambapo kufikia mwaka huo familia ya Gnassingbé itakua imekaa madarakani kwa muda wa miaka 63.