Sahle azuru Kenya

0
481

Rais Sahle-Work Zewde wa Ethiopia yupo nchini Kenya kwa ziara ya siku moja, ikiwa ni ziara yake ya kwanza ya kikazi nchini humo tangu ateuliwe kushika wadhifa huo mwezi Oktoba mwaka 2018.

Lengo la ziara hiyo ni kukutana na Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya na kujadili ushirikiano baina ya nchi hizo mbili pamoja na ushirikiano na nchi jirani na nchi hizo.

Kwa muda mrefu Ethiopia na Kenya zimekua zikishirikiana katika kukabiliana na biashara za mpakani zinazoendeshwa kinyume cha sheria na nchi zote hizo zimepeleka vikosi vyake nchini Somalia kwa lengo la kusaidia ulinzi wa amani.