Safari ya Biden na Kamala White House

0
247

Raia wa Marekani pamoja na wale wa Mataifa mengine duniani, wanaendelea kusubiri kwa hamu tukio la kuapishwa kwa Rais Mteule wa Marekani, – Joe Biden na Makamu wake Kamala Harris.

Sherehe za kuapishwa kwa Viongozi hao zinafanyika jijini Washington na zitahudhuriwa na watu wachache kutokana na hofu ya mlipuko wa virusi vya Corona.

Sherehe hizo hazitahudhuriwa na Rais anayemliza muda wake Donald Trump, na badala yake Trump ametoa hotuba yake ya mwisho katika kambi ya kijeshi ya Andrews muda mfupi mara baada ya kuondoka White House.

Marais Sita Wastaafu wa Marekani wanatarajiwa kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais huyo wa 46 wa Marekani, -Joe Biden na Makamu wake Kamala Harris.

Kamala Harris ambaye anakuwa Mwanamke wa kwanza kushika wadhifa wa Makamu wa Rais wa Marekani, ndiye atakayeapishwa wa kwanza na ndipo atafuata Biden.