Rwanda yathibitisha visa 6 vya Omicron

0
184

Rwanda imethibitisha visa sita vya maambukizi ya virusi vya UVIKO19 aina ya Omicron, wizara ya afya ya nchi hiyo imeeleza.

Visa hivyo vimebainika katika sampuli zilizokusanywa kutoka kwa wasafiri na watu waliokutana nao.

Baada ya hali hiyo wizara imehimiza wale wote wenye umri kuanzia miaka 12 kupata chanjo, na wale wenye miaka 18 au zaidi kupata chanjo ya pili (booster).

Hadi sasa Rwanda imechanja takribani asilimia 40 ya watu wake na imeanza kutoa chanjo kwa mzunguko wa pili.