William Ruto ameapishwa kuwa Rais wa tano wa Taifa la Kenya.
Ruto ameapishwa kuwa Rais wa Kenya kufuatia ushindi alioupata katika uchaguzi mkuu wa nchi hiyo uliofanyika Agosti 9 mwaka huu akitokea muungano wa Kenya Kwanza.
Jaji Mkuu wa Kenya, Martha Koome ndiye aliyemuapisha Ruto pamoja na Naibu Rais Rigathi Gachagua.
Marais kutoka nchi 16 za Afrika akiwemo Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania wanashiriki katika sherehe za kuapishwa kwa William Ruto katika uwanja wa Kasarani jijini Nairobi.
Sherehe hizo pia zimehudhuriwa na raia elfu 60 wa Kenya pamoja na viongozi mbalimbali kutoka mashirika ya kimataifa na mabalozi.